DOGO ANAYEPIGA KAZI KINYEMELA KWA NYOSH EL SADAAT AIANGUKIA KAMPUNI YAKE

SIKU chache baada ya mtandao huu kuandika taarifa za mwimbaji Kelly Haso kusemekana kukiuka mkataba wa kampuni ya Nyegera Waitu alioingia kuitumikia na kujiunga kinyemela na bendi ya Bogoss Musica ya Nyosh El Sadaat, hatimaye mwafaka umefikiwa.

Kelly Hasso akiwa kaambatana na baba yake mzazi, baada ya taarifa ile walimwendea mkurugenzi wa Nyegera Waitu, tabibu Ntamba na Mungu na kumuomba msamaha ambapo kilichotokea ni Ntamba na Mungu kutoa baraka Kelly akafanye kazi na Nyosh.

Muda mfupi uliopita, Ntamba na Mungu ameongea na Saluti5 na kusema kuwa amemruhusu Kelly kupiga mzigo ndani ya Bogoss kwa sharti la kutojiunga moja kwa moja na bendi hiyo kwa kuwa bado ana mkataba ndani ya Nyegera Waitu.


“Tumeshamalizana na Kelly. Alikuja na wazazi wake tukazungumza nao kwa pamoja, ila kwa kifupi kampuni imemruhusu kuendelea na Bogoss kwa sharti la kutosaini nao hadi hapo mkataba wake na sisi utakapomalizika ndipo atakapoamua mwenyewe,” amesema Ntamba.  

No comments