FATHER MAUJI ASEMA "MNAOOMBEA YAH TMK IFULIE MTANGOJA SANA"

YAH TMK Modern taarab juzi wamesherehekea kutimiza mwaka mmoja tangu kuasisiwa kwa bendi yao na mmoja wa viongozi wao waandamizi, Mohammed Mauji amenena mazito.

Mauji amesema kuwa kwake yeye ni faraja kubwa sana kufikia hatua hiyo kwani itakuwa wamewafunga kidomodomo wale wote ambao walikuwa wakiwatabiria kutokufika mbali katika mbio za uburudishaji.

“Binafsi naamini katika maisha nidhamu na kujituma ndio msingi wa maisha yako, pia unatakiwa wewe mwenyewe kwanza ukiamini kile kitu ambacho unakifanya kwa kujua siku za mbeleni kitakuja kukupa manufaa na usiangalie nani anasema nini kwani miluzi mingi humpoteza mbwa,” amesema Mauji. 


“Kwa upande wetu mwanzo ulikuwa mgumu sana na wapo waliosema hatutafika popote, lakini kwakuwa tulikuwa tunakiamini kile tunachokifanya tulikubali kuvumilia yote kwa pamoja na hatimaye huu ni mwaka sasa.” 

No comments