FATMA MCHARUKO AANIKA TOFAUTI YAKE NA MASUPASTAA WENGINE WA KIKE

MWANAMIPASHO Fatuma Mcharuko amesema kwamba tofauti yake na masupastaa wengi wa kike, hususan waimbaji taarab ni kwamba hana majivuno kwa mashabiki anaowatumikia.

Akipiga stori na Saluti5, Mcharuko anayetamba sasa na kibao “Siwaguni Siwakohoi” akiwa na bendi ya Yah TMK Modern Taarab, amesema kwamba anatambua umuhimu wa mashabiki hivyo lazima aweke heshima kwao.

“Kwa kawaida yangu sina maringo kwa mashabiki, hiyo ndio tofauti yangu kubwa na masupastaa wengine wakiwemo waimbaji wenzangu, nasikiliza sana maoni na kuyafanyia kazi,” amesema Mcharuko.


“Namuheshimu pia mume wangu na simvunjii heshima kwani yeye ndie anayeniongoza katika masuala yote ya kimaisha kwa sasa na ndio maana nafanikiwa kwa kiasi kikubwa bila kukwama,” ameongeza msanii huyo.

No comments