GIGGY MONEY ASEMA KWA MWANAUME ANAFUATA PENZI LA KWELI SIO PESA

MKALI wa kibao “Nampa Papa”, Giggy Money ameweka wazi kuwa huwa haangalii mshiko katika masuala ya mahusiano bali anachojali yeye ni kuona kwamba anatua kwenye mikono salama ya mwanaume mwenye mapenzi ya kweli.

“Kama utaweka pesa mbele unaweza kukutana na mwanaume mwenye mapungufu kibao kisha mwenyewe ukajikuta unajuta, hivyo ni bora uchague tu kuwa na mwanaume mwenye real love,” amesema Giggy.


“Mwanaume wangu mimi sio maarufu kusema labda anajulikana, sio tajiri hapa mjini kuweza kushindana na matajiri tunaowajua, sio handsome na wala hana jina hata kidogo, mimi wa mjini enough nikipata wa mjini mwenzangu tutaumizana vichwa,” ameongeza.

No comments