HAJI ADAM WA BONGOMUVI AGEUKA “DANGA”

BAADA ya kubaini kuwa mume wake ana tatizo la kushindwa kushiriki kikamilifu tendo la ndoa, Grace anaanza kutoka nje kwa kumtafuta mwanaume mashine ambaye anapomkoleza kimahaba anachukua hatua ya kumhonga mali za mumewe ikiwemo pesa na gari.

Hayo yamo ndani ya muvi mpya ya Kibongo inayokwenda kwa jina la “Danga” ambayo ndani yake unampata nguli wa hisia za mapenzi katika filamu, Haji Adam “Baba Haji” anayeinogesha zaidi kwa “kulialia” kama ilivyo kawaida yake.

Kampuni ya Joh Film ya jijini Dar es Salaam ndio wanaoshusha ambacho mbali ya Baba Haji, pia kimekusanya mastaa wengine kibao wakiwemo Said Kahunda na Grace Michael.


Msemaji wa Joh Film, Isihaka Mkali ameiambia Saluti5 kuwa mzigo utatupwa sokoni mwishoni mwa mwezi huu ambapo wanaamini watafunika vilivyo kutokana na namna kazi yenyewe ilivyosimama.

No comments