HASSAN MOSHI ASHUSHA RAPU MPYA YA "MAMA ASHURA"

MWIMBAJI Hassan Moshi wa Msondo Ngoma Music Band ameibuka na rapu mpya inayokwenda kwa jina la “Mama Ashura” ambayo ameanza kupagawisha nayo kwenye kumbi mbalimbali wanazotumbuiza.


Katika maonyesho ya Msondo Ngoma ya mwishoni mwa wiki kwenye kumbi za Dar Safari Park, Buza na Bulyaga Temeke, jijini Dar es Salaam, Saluti5 imeshuhudia namna mashabiki wanavyomiminika kati kwa wingi kucheza kila pale Hassan anavyoianzisha rapu hiyo.

No comments