HASSAN MOSHI AWATULIZA MASHABIKI WA MSONDO NGOMA WANAOTAMANI UJIO WAKE

HASSAN Moshi William amesema anatambua kwamba mashabiki wa Msondo Ngoma wana hamu ya kuona anaporomosha nyimbo ndani ya bendi hiyo ili kuendeleza pale alipoachia baba yake, lakini akawatuliza mzuka kwa kusema kuwa mambo mazuri hayataki haraka.

Hassan ambaye ni kati ya watoto wa marehemu Moshi William aliyekuwa mwanamuziki mwandamizi wa Msondo Ngoma, ambaye anaonekana kufuata vilivyo nyayo za mzee wake huyo, amesema hautapita muda mrefu kabla hajawapa faraja wapenzi wao.


“Nafahamu matakwa na kiu kubwa ya mashabiki wangu pamoja na wale waliokuwa wanamfuatilia mzee kwa karibu zaidi, lakini bado kidogo najipanga na muda si muda nitaanza kuwaibulia vitu vitakavyorudisha nyuma hisia zao enzi za baba yangu,” amesema Hassan.

No comments