Habari

HATIMAYE COUTINHO MALI YA BARCELONA, USAJILI WA PAUNI MIL 145 WAKUBALIKA, APEWA MKATABA WA MIAKA MITANO

on

Hatimaye Philippe Coutinho amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Barcelona kutoka Liverpool kwa pauni milioni 145. 

Kiungo mshambuliaji huyo wa Kibrazil ameingia mkataba wa miaka mitano na nusu kuitumikia Barcelona, klabu ya njozi yake.

Katika dili hilo, Barcelona imeweka kipengele cha manunuzi cha pauni milioni 335 kwa klabu itakayotaka kumsajili kabla mkataba wake haujaisha.

Coutinho anakuwa mchezaji wa pili ghali duniani akitanguliwa na Mbrazil mwenzake Neymar aliyesajiliwa na PSG kwa paunu milioni 198 kutokea Barcelona kiangazi kilichopita.

Liverpool wametengeneza faida kubwa kwa mchezaji waliyemnunua kwa pauni 8.5 kutoka Inter Milan mwaka 2013.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *