HUSSEIN JUMBE AONGEZA MAJONZI MSIBA WA LIMONGA JUSTINE

NGULI wa muziki wa dansi, Hussein Jumbe amejikuta akiwaongezea simanzi mamia ya waombolezaji waliokusanyika kuuaga mwili wa aliyekuwa mwanahabari wa Uhuru Fm, Limonga Justine, baada ya kuimba kwa hisia kali wimbo maalum kumuhusu marehemu huyo.

Ibada ya kuaga mwili wa Limonga imefanyika jana mchana katika viwanja vya Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wanafamilia ya habari, wasanii pamoja na wadau tofauti tofauti.

Katika wimbo huo uliokuwa umejaa mashairi ya simanzi na majonzi, Jumbe amemtaja Limonga kama mtu ambaye alikuwa akijitoa vilivyo katika masuala ya kijamii na ambaye alithubutu na kumudu kuwa karibu na aliokuwa akiwatumikia ambao ni wanajamii wenyewe.

Limonga alifariki dunia Desemba 30, mwaka jana katika hospitali ya TMJ alikolazwa akitibiwa na ameacha mjane na watoto wawili ambapo mazishi yake yamefanyika katika makaburi ya Saku yaliyopo Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

No comments