IBRAHIM KANDAYA: SIJUI KWANINI TX MOSHI ALINIPA JINA LA "PROFESA"

MCHARAZAJI mahiri wa gitaa zito la Bass, Ibrahim Kandaya amesema hafahamu kwanini marehemu Tx Moshi William aliamua kumpachika jina la “Profesa” tangu siku ya kwanza alipokutana nae.

Kwa mara ya kwanza Moshi na Kandaya walikutana mwaka 2002 walipokuwa wakiandaa nyimbo za bendi ya zinzong iliyokuwa imekusanya wasanii kama vile; Adolf Mbinga, Michael Liloko, Victor Mkambi, Salleh Kupaza, Roggat Hegga, Suleiman Mbwembwe na Shomary Ally.

Akiongea na Saluti5, Kandaya aliyewahi kuitumikia Msondo Ngoma ambayo pia alikuwa akiimbia Moshi Wiliam, amesema anasikitika kuona mkongwe huyo amekufa kabla hajamueleza kilichosababisha ampe jina hilo.

“Nilipokutana nae kwa mara ya kwanza tu yule brother alinambia kuwa lazima anivute Msondo Ngoma ingawaje alijua kwamba niko Nchinga Sound wakati huo na papohapo akanipa jina la “profesa” ambalo kiukweli natamani sana kujua maana yake,” ameswema Kandaya.


Kandaya aliingia Msondo Ngoma mwaka 2003 na kuondoka takriban miaka miwili nyuma akiwa kashiriki kurekodi albamu tano ambazo ni “Piga Ua Talaka Utatoa”, “Kaza Moyo”, “Ajali”, “Kicheko” na “Huna Shukrani”. 

No comments