Habari

JESSE LINGARD HII SASA SIFA, KILA MECHI BAO!!!!

on

Wakati Jesse Lingard aliposaini mkataba mpya mwezi April unaomwingizia pauni 100,000 kwa wiki, mashabiki wengi wa Manchester United hawakuridhika na waliona kama vile mshambuliaji huyo amekuzwa kupita maelezo.
Lakini sasa Lingard mwenye umri wa miaka 25 anawathibitishia kwa vitendo kuwa yeye ni mchezeshaji timu na mfungaji.
Goli lake la nane ndani ya michezo 1o iliyopita, lilikuwa chachu ya Manchester United kuvuna ushindi wa 2-0 dhidi ya Derby County kwenye mchezo mgumu wa mzunguko wa nne wa FA Cup.
Magoli yote mawili ya United yalikuja katika dakika 10 za mwisho ambapo Lingard alifunga bao lake dakika ya 85 huku Romelu Lukaku akifunga la pili dakika ya 90.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *