Habari

JONNY EVANS ALIYETOSWA NA MANCHESTER UNITED SASA AGEUKA LULU, KLABU KUBWA ZAMGOMBEA

on

Mwaka 2015 ilionekana kama vile Jonny Evans si mali kitu pale Manchester United  kuumuza kwa bei ya kutupa kwenda West Bromwich Albion, lakini beki huyo sasa amekuwa kimbilio la vilabu vikubwa.
Vilabu kadhaa vikiwemo Arsenal na Manchester City vimeonyesha nia ya kutaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa pauni milioni 25.
Arsenal wana nafasi nzuri zaidi ya kushinda vita hivyo kwani West Brom wanamtaka beki wa kushoto Mathieu Debuchy, 32, ambaye anatafuta fursa ya kuchezwa kikosi cha kwanza.
City wanataka mchezaji wa kujaza nafasi ya nahodha Vincent Kompany ambaye ameumia tena.
Manchester United nao wanatajwa kusaka saini ya beki huyo waliyemuuza kwa pauni milioni.
Klabu nyingine za Ligi ya Premia pia zinamtaka Evans lakini haziwezi kushindana na klabu ambazo zinacheza soka ya Ulaya.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *