JOSE MARA ASEMA BONGO HAKUNA MWIMBAJI WA KUMUUMIZA KICHWA

MWIMBAJI Jose Mara ameibuka na kusema kwamba kwa hapa Tanzania hakuna mwanamuziki anayeweza kumshinda kiuimbaji ila amekiri kuwa wapo wenye uwezo mkubwa wa sauti jukwaani.

Akiongea na Saluti5, Jose amesema kwamba anaheshimu mchango wa waimbaji kama vile; Ally Chocky, Nyosh El Sadaat, King Blaize, Alphabet Kabeza, Salleh Kupaza, Pablo Masai na wengineo ambao vipaji vyao vya sauti vinaliongezea dansi mashabiki.

“Kiukweli hakuna anayeniumiza kichwa katika uimbaji ila sikatai wapo wale ambao wanaimba vyema haswa,” amesema bosi huyo wa bendi ya Mapacha Watatu.

No comments