Habari

JUMA KATUNDU WA MSONDO NGOMA AKUMBUSHA “UDUGU MALI YA MUNGU”

on

MMOJA wa viongozi waandamizi na
mwimbaji tegemeo ndani ya Msonmdo Ngoma Music Band, Juma Katundu amewaandalia
mashabiki wake zawadi ya mwaka mpya 2018, ambayo ni kete iitwayo “Udugu mali ya
Mungu”, imefahamika.
Akiongea na Saluti5, Katundu
amesema kuwa “Udugu Mali ya Mungu” ni kibao anachoamini kwamba kitateka vilivyo
nafsi za mashabiki kutokana na kukitunga umakini mkubwa huku kikiwa kimesheheni
mashairi yenye ujumbe mzito.
“Hii ni kama zawadi ya mwaka
mpya wa 2018 kwa mashabiki wa Msondo Ngoma baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu
kidogo sasa nimeamua kuwaletea kitu balaa,” ametamba Katundu.
Amesema kuwa hivi sasa anamalizia
kukiandaa kibao hicho kabla hajakiwasilisha mazoezini na kuanza kukipika rasmi
wakiwa pamoja na wanamuziki wenzie wa Msondo Ngoma.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *