KAMARADE ALLY CHOCKY AITWA IVORY BAND... kuwasha moto Ngasa Pub Kimara usiku huu

IVORY Band chini ya Rama Pentagone, Rashid Sumuni na Omary Kisila usiku wa leo inatarajiwa kumimina burudani kali ndani ya Ngasa Pub, Kimara Gorani jijini Dar es Salaam sambamba na Ally Chocky atakayepanda jukwaani kama msanii mwalikwa, imefahamika.

Rama Pentagone ameiambia Saluti5 kuwa, shoo imepangwa kuanza kurindima majira ya saa 2:00 usiku na kuendelea hadi muda mbaya ambapo watakaohudhuria watafaidi mambo matamu ikiwa ni pamoja na vibao vipya kutoka kwao.

“Kwa upande wa Chocky ana vibao vingi vikali hivyo mashabiki wetu watarajie kupata nyimbo bomba kutoka katika bendi zote ambazo amewahi kuzitumikia bila kusahau ile ya Extra Bongo ambayo nilikuwa nae,” amesema Pentagone.

No comments