KUMBE KAMA SI MUZIKI BITCHUKA ANGEKUWA "RONADINHO" WA BONGO


NGULI wa uimbaji kutoka Mlimani Park Sikinde, Hassan Rehani Bitchuka amebainisha kwamba, inawezekana isingekuwa muziki basi angekuwa mwanasoka kutokana na kuwa hiyo ndio ilikuwa fani yake kubwa huko nyuma.

Bitchuka ambaye amekiri kuwa ni mnazi mkubwa wa timu ya Simba ya Mtaa Msimbazi, Dar es Salaam na Manchester United ya Uingeleza, amesema kwamba aliwahi kuchezea timu ya Tusker FC ya jijini Arusha.

“Nimecheza sana mpira na hadi sasa bado naupenda sema nsdio hivyo tena nishaingia kwenye majukumu mengine ya muziki na umri nao ushakwenda, ila mimi ni Simba damu,” amesema nguli huyo mwenye sauti kali isiyochusha.

No comments