LEO NDIO LEO AL-JAZEERA NDANI YA SPLENDID HALL TANGA

BENDI ya taarab ya Al-Jazeera baadae leo inatarajiwa kukinukisha ndani ya Splendid Hall, jijini Tanga katika shoo iliyopangwa kuanza kuunguruma majira ya saa 3:00 usiku na kuendelea hadi majogoo.

Shoo hiyo maalum kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2018, inafanyika usiku wa leo baada ya kughahirishwa jana kutokana na sababu za kiusalama.


Taarifa kutoka ndani ya Al-Jazeera zinasema kuwa kiingilio katika shoo hiyo ni kuwa sh. 4,000 ambapo mashabiki watakaobahatika kuhudhuria watafaidi burudani pevu itakayoambatana na vibao mbalimbali vya “old is gold”.  

No comments