MADEBE LIDAI AJA NA FILAMU YA “MWENYEKITI”... kuimimina sokoni Januari 15

MKALI wa filamu za Kibongo aliyeibuka kuwa gumzo kubwa kwa sasa, Madebe Lidai ambaye anafahamika zaidi kwa jina la “Nabii Mswahili” yuko mbioni kuonekana kwenye kazi mpya inayokwenda kwa jina la “Mwenyekiti”.

Katika muvi hiyo inayoandaliwa na kampuni yake ya LP Media, Madebe amewaasa watu waendelee kukazana kwa nia njema dhidi ya taifa lao bila kuangalia jinsia, kwenye masuala ya kilimo, elimu pamoja na kuzidi kutafuta hitaji sahihi la mioyo yao.


Ndani ya “Mwenyekiti” ambayo imepangwa kumwagwa rasmi mtaani Januari 15 , mwaka huu, Madebe amecheza na wakali wengine kadhaa wanaofanya poa hivi sasa kwenye gemu la filamu, wakiwemo Hashimu Omary na Khadija Minah. 

No comments