MAJAMBAZI YAVUNJA SHOO YA VICTORIA SOUND MBAGALA

SHOO ya Victoria Sound ndani ya Kiburugwa Inn, Mbagala Kiburugwa, jijini Dar es Salaam jana Jumapili ililazimika kukatishwa kabla ya muda wake baada ya majambazi wenye silaha kuvamia duka la vyakula jirani na ukumbi huo na kumuua mwuzaji.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 3:45 ambapo majambazi hao wanaokadiliwa kuwa zaidi ya wanne kabla hawajampiga risasi shingoni mwuzaji huyo, walianza kuzitawanya ovyo juu wakati wa mvutano kati yao wakimtaka awapatie fedha.


Kutokana na hofu kubwa, muziki wa Victoria Sound ambao ndio kwanza ulikuwa unaanza kukolea ndani ya Kiburugwa Inn, ulizimwa gafla na uongozi wa ukumbi kuamuru dansi liahirishwe hadi wiki ijayo wakihofia usalama.

No comments