MALCOM ATAKA KUJIUNGA NA ARSENAL, HANA MPANGO NA TOTTENHAM


Winga wa Kibrazil, Malcom yupo tayari kuichagua Arsenal na kuitosa Tottenham.
Malcom anayeitumikia Bordeaux, anatakiwa na timu nyingi zikiwemo Arsenal, Tottenham na Manchester United.
Ingawa ripoti kutoka Brazil zinadai vilabu vyote hivyo vimeshakutana na wawakilishi wa Malcom lakini mchezaji huyo anapendelea zaidi kwenda Emirates.
Kocha wa Arsenal, Wenger amekataa kufunguka juu ya mbio zao za kumsaka Malcom ambapo alisema: "Ni mchezaji mzuri lakini hatupo kwenye mbio hizo. Kwasasa hatuna hatua yoyote tuliyofanya juu yake".

No comments