MANCHESTER CITY HAINA KUREMBA, KOMBE LOLOTE WANAFANYA KWELI …waichapa Bristol City 2-1 na kunusa fainali ya EFL (Carabao Cup)


Manchester City wametanguliza mguu mmoja kwenye fainali ya Carabao Cup ambayo msimu uliopita ilijulikana kama EFL Cup.

Vijana wa Pep Guardiola ambao ni wazi kuwa msimu huu wamepania kusepa na mataji yote, wakawafunga wababe wa Manchester United - Bristol City 2-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali.

Timu hizo zitarudiana Januari 23 ambapo kama Manchester City itasonga mbele basi katika mchezo wa fainali itakutana na mshindi kati ya Arsenal na Chelsea.

Bristol City ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 44 lililokuja kwa njia ya penalti mfungaji akiwa ni Bobby Reid.

Manchester City ikasawazisha dakika ya 55 kupitia kwa Kevin De Bruyne kabla Sergio Aguero hajatupia bao la ushindi dakika ya 90.

MANCHESTER CITY (4-2-3-1): Bravo 6.5; Danilo 6, Stones 5, Mangala 5, Zinchenko 6; Toure 6 (Aguero 69mins 6), B Silva 6, Gundogan 6, De Bruyne 7.5, Sane 6.5; Sterling 7.

BRISTOL CITY (4-4-2): Fielding 8; Wright 7, Flint 7.5, Baker 7.5, Magnusson 7 (Walsh 72mins 6); Brownhill 6.5, Pack 6.5, Smith 7, Bryan 7; Paterson 7, Reid 7.

No comments