Habari

MANCHESTER CITY YABISHA HODI ARSENAL NA OFA YA PAUNI MIL 30 KWAAJILI YA ALEXIS SANCHEZ

on

Manchester City imefungua maongezi na Arsenal kwaajili ya kupata saini ya Alexis Sanchez kwa pauni milioni 30.

Vigogo wa Etihad wamefanya mawasiliano na Arsenal ili kujua kama dili hilo linaweza kufanyika dirisha hili la usajili la Januari.
Kocha wa Manchester City anataka kuongeza mshambuliaji mpya baada ya hivi karibuni Gabriel Jesus kuumia  na kubainika kuwa atakuwa nje ya dimba kwa miezi miwili.

City walikuwa na matumaini ya kumsajili Sanchez kwa uhamisho huru majira ya kiangazi lakini sasa wameamua kuingia sokoni mapema ili kujaribu kumnunua nyota huyo wa kimataifa wa Chile ambaye amekataa kusaini mkataba mpya Arsenal.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *