MANCHESTER CITY YAREJEA KWENYE ANGA ZAKE ZA USHINDI, TOTTENHAM NAYO YAPAA, WEST HAM MAMBO SWAAFI


Manchester City imerejea kwa kishindo kwenye anga zake za ushindi kwa kuichakaza Watford 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kwenye dimba la Etihad.

Jumapili iliyopita City ilipunguzwa kasi na Crystal Palace kwa kulazimishwa sare ya 0-0, lakini Jumatano usiku ikafanikiwa kunyakua pointi tatu kwa Watford na kujitanua kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi 15.

City ambayo bado haijapoteza mchezo wa Ligi Kuu msimu huu, ilipata bao lake la kwanza sekunde ya 38 kupitia kwa winga Raheem Sterling akiunganisha krosi tamu ya Sane.

Bao la pili la City liliwadia dakika ya 13 baada ya beki Christian Kabasele kujifunga katika juhudi zake za kuokoa kwaju wa Kevin De Bruyne.

Sergio Aguero akafunga goli la tatu dakika ya 63 huku
Andre Gray akiifungia Watford bao la kufutia machozi dakika ya 83.

Haya ndiyo matokeo ya mechi zote zilizochezwa Jumatano usiku:
Southampton 1 - 2 Crystal Palace
Swansea City 0 - 2 Tottenham Hotspur
West Ham United 2 - 1 West Bromwich Albion

Manchester City 3 - 1 Watford

No comments