Habari

MANCHESTER UNITED YAKUBALIANA NA LUCAS MOURA WA PSG …Mourinho asema atakidhi mahitaji yao ya winga

on

Manchetser United imekubaliana juu ya maslahi banafisi na winga wa PSG Lucas Moura ambaye alikataa ofa ya kwenda Old Trafford chini ya Sir Alex Feruguson mwaka 2012.
Kwa mujibu wa gazeti la Gazzetta dello Sport la Italia nyota huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25, amebakiza siku chache kabla ya kujiunga na Manchester United katika dirisha la usajili la mwezi huu wa Januari.
Licha ya kuelezwa kuwa bado Manchester United haijaweka mezani ofa yao, lakini tayari inadaiwa PSG wako tayari kumaliza biashara kwa dili la pauni milioni 35.
Kocha wa Manchester United ni kama vile ameushinikiza kiana uongozi wa klabu hiyo kuharakisha usajili wa Moura.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mourinho ameandika kuwa kama ni kweli Moura yuko sokoni kwa euro 20 – 25 kwa soko la sasa, hiyo ni biashara nzuri sana na kama watamsajili basi ataongeza nguvu na kukukidhi mahitaji yao ya winga.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *