MASSIMILIANO ALLEGRI AKUBALI KUMRITHI ANTONIO CONTE CHELSEA


Massimiliano Allegri anaongoza orodha ya makocha wanaotajwa kumrithi Antonio Conte Chelsea na inaaminika ameshakubali kwenda Stamford Bridge.

Wakati Conte anatarajiwa kuondoka kwa mabingwa hao wa Premier League mwishoni mwa msimu huu, ripoti kutoka Italia zinadai Allegri kocha wa Juventus ndiye chaguo kuu la Chelsea.

Gazeti la Corriere dello Sport la Italia linadai Allegri ndiye anayetarajiwa kumrithi Conte kama alivyomrithi ndani Juventus mwaka 2014.
No comments