Habari

MOURINHO AANZA KUCHOSHWA NA UBAHILI WA MANCHESTER UNITED KWENYE USAJILI WA DIRISHA DOGO

on

Jose Mourinho ameanza kushindwa uvumilivu kwa namna Manchester United inavyochelewa kupeleka ofa ya pauni milioni 40 ili kumsajili beki wa kushoto wa Tottenham Danny Rose.
Mourinho anamtaka beki huyo mwenye umri wa miaka 27 ili kutibu tatizo la safu yake ya ulinzi.
Hata hivyo, bodi ya United inaamini beki Luke Shaw aliyesajiliwa kwa pauni milioni 30 kutoka Southampton mwaka 2014, bado ana nafasi ya kubwa beki bora wa kushoto licha ya kuandamwa na tatizo la kuwa majeruhi mara kwa mara.
Hatua hiyo inatishia kutibua mahususiano ya bodi ya Manchester United na Mourinho ambaye alishaweka wazi kuwa klabu yake bado inahistaji kufanya usajili wa kishindo iwapo inataka kuchuana na Manchester City.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *