Habari

MOURINHO ASEMA USAJILI JANUARI NI MUHIMU MANCHESTER UNITED ILA SIO LAZIMA

on

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema upo umuhimu wa kusajili wachezaji wapya kwenye kikosi chake dirisha hili la Januari lakini akasema atakuwa mpole pale jambo hilo litakaposhindikana.
Manchester United ilitakata kwenye dimba la Goodison Park dhidi ya Everton Jumatatu usiku licha ya kuwakosa nyota wake kibao wakiwemo Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly, Antonio Valencia, Ashley Young, Chris Smalling, Marouane Fellaini na Michael Carrick.
Mourinho akaiambia Sky News: “Sijui lolote kuhusu usajili.
“Kwasasa tuko matatizoni, pengine baada ya wiki mbili au tatu tutaimarika. Siwezi kusema lolote kuhusu usajili, sijui kama tutaongeza wachezaji wapya au la.
“Kama ataongezeka mchezaji mpya itakuwa jambo jema lakini kama hatapatikana nitasubiri hadi dirisha la kiangazi na tutapigana kwa kikosi tulichonacho”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *