Habari

MOURINHO KUBAKIA MANCHESTER UNITED HADI MWAKA 2021 IWAPO ATAAHIDIWA FUNGU LA USAJILI

on

Jose Mourinho atasaini mkataba mpya Manchester United na kubakia hadi mwaka 2021 – iwapo tu klabu hiyo itabadilisha sera zake za usajili.
Bosi huyo wa United hana furaha na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward  kwa namna anavyosita kutoa pauni milioni 80 za usajili wa dirisha dogo.
Mourinho anataka awe na sauti juu ya pesa za kumwaga kwenye usajili na juu ya mchezaji gani anunuliwe.
Hivi karibuni Mourinho alilalamika kuwa pauni milioni 300 alizotumia kwenye usajili tangu atue Manchester United, hazitoshi kuleta mataji.
Kocha huyo anataka kusaji beki wa kushoto kati ya Danny Rose wa Tottenham, Ryan Sessegnon wa Fulham au Kieran Tierney wa Celtic.
Mourinho pia anamtaka beki wa kulia Fabinho na kiungo Thomas Lemar wote wa Monaco sambamba na winga wa Bordeaux Malcolm.
Inaaminika Woodward na bodi yake imemwambia Mourinho kuwa hawaoni hekima kumwaga pesa nyingi dirisha hili la usajili na hasa kutokana na ukweli kuwa matumaini ya kufukia pengo la pointi 15 la Manchester City, ni madogo mno. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *