MSONDO NGOMA KAMA KAWA DAR SAFARI PARK LEO... "surprise" za kufa mtu zimeandaliwa kwa mashabiki

BABA ya Muziki, Msondo Ngoma Music Band kama ilivyo kawaida yao kwa siku za Jumamosi, baadae leo wataporomosha burudani kali ndani ya Dar Safari Park, Buza, jijini Dar es Salaam.

Mirindimo itaanza mishale ya saa 2:30 usiku na kuendelea hadi majogoo ambapo mpya na zile kali tupu za zamani zinatarajiwa kumiminwa kwa mashabiki huku maombi yakipewa kipaumbele zaidi.


Taarifa kutoka ndani ya bendi hiyo zinasema kuwa shoo ya leo inatarajiwa kujaa msisimko wa hali ya juu kutokana na mambo mengi matamu pamoja na surprise kibao zilizoandaliwa.

No comments