MZEE MSISILI AWAITA WASANII CHIPUKIZI "KUPIGA MZIGO"

MKONGWE wa sanaa ya filamu Bongo, Fadhili Msisili amewaita wasanii chipukizi kuanza kufanya kazi nae mwaka huu mpya wa 2018, lengo likiwa kuinua na kukuza vipaji vya wasanii wachanga hapa Bongo.

Akiongea na Saluti5, Msisili amesema kuwa  anatarajia kuanza kuingia kazini muda si mrefu na amewachagua zaidi wasanii chipukizi, ili kuhakikisha anakuwa mmoja wa watu watakaoacha sifa kwa kuibua vipaji.

“Yeyote anayejijua ana kipaji cha sanaa au anayetaka kuifahamu sanaa anitafute. Nathamini sana watu ambao wana nia na sanaa, hususan wale wanaochipukia,” amesema mkongwe huyo ambaye ni mahiri kwa muvi za kitamaduni.


“Kama unatokea kwenye kundi lako unalolitumikia, itabidi uanze kuniletea barua kutoka huko kundini kwako ya kukuruhusu kufanya kazi nje nami nitakupokea bila kipingamizi,” ameongeza.

No comments