NAIROBI, MOMBASA WAITAKA TENA SIKINDE NGOMA YA UKAE

MASHABIKI wa muziki wa dansi nchini Kenya wamewaita tena Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae” kuwaburudisha, ikiwa ni miezi minne tu tangu wakongwe hao kufanya ziara ya mafanikio nchini humo.

Mara ya mwisho Sikinde walizuzuru Kenya Septemba, mwaka jana na kufanya maonyesho kwa wiki moja katika mji wa Nairobi ambapo walikubalika vilivyo, kwa mujibu wa kiongozi wao mwandamizi, Abdallah Hemba.

“Tunasubiri tu uhakika wa kiusalama kutokana na hali ya kiasiasa ilivyo huko Kenya kwa sasa. Ila safari hii tunatarajia kuzuru mikoa mingi zaidi kwani tumepokea pia maombikutoka katika mikoa mingine kadhaa,” amesema Hemba.


Hemba amesema kuwa ziara hiyo imeandaliwa na promota maarufu nchini humo aliyemtaja kwa jina la Madame Akinyi.

No comments