NASSOR DIMOSO: ASANTENI WAKAZI WA MWANZA, TULIENI MTATUSOMA TU

BOSI wa 4 Stars Band, Nassor Dimoso amewashukuru wakazi wa jijini Mwanza kwa kujitokeza kwa wingi kwenye shoo yao maalum ya kuukaribisha mwaka mpya iliyorindima Jumapili ndani ya viwanja vya Buzuruga.

Dimoso ameiambia Saluti5 kwa njia ya simu kuwa sapoti walioionyesha mashabiki wa Mwanza katika shoo hiyo ya mwisho kwa mwaka jana imewafariji kupindukia hivyo ameahidi kuzidi kuwapa mambo matamu zaidi mwaka huu.

“Tuko hapa jijini Mwanza kwa karibu mwaka mmoja sasa na kwakweli tumekuwa tukifarijika na sapoti ya mashabiki wa huku, lakini tukio la kujitokeza kwa wingi siku ya mkesha limetuongeza mori zaidi, hivyo nasi hatuna budi kulipa fadhila kikamilifu,” amesema Dimoso.

“Tunawaambia mashabiki wetu kwamba wasubiri mambo matamu yanakuja muda si mrefu ambayo si mengine bali ni vibao vyao vipya pamoja na shoo ya kufa mtu.”

No comments