Habari

PAUNI MIL 133 KUMNG’OA COUTINHO LIVERPOOL MWEZI HUU …safari ya Barcelona imeiva

on

Barcelona wanatarajiwa kuweka mezani pauni milioni 133 ili kumsajili staa wa Liverpool Philippe Coutinho mwezi huu.
Vyombo vya habari vya Hispania vinaamini kuwa Coutinho hatavaa tena jezi ya Liverpool msimu huu.
Coutinho aliukosa mchezo wa Jumatatu wa ushindi wa 2-1 dhidi ya Burnley kufuatia maumivu ya paja lakini Jumanne aliwasili kwenye ngome yao ya Melwood kwaajili ya matibabu na hatarajiwi kushiriki mechi ya FA dhidi ya Everton Ijumaa jioni.
Barcelona ilijaribu kumsajili Countinho bila mafanikio dirisha la kiangazi ambapo ofa yao ya juu kabisa ya pauni milioni 114 ilipigwa chini.
Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanaamini Liverpool haitendelea kumng’ang’ania mchezaji ambaye hana utashi wa kuitumikia klabu siku za usoni.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *