PICHA 30: MASHAUZI CLASSIC WALIVYOITEKA KILWA, LINDI, MASASI NA LIWALE


Kundi la Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi “Jike la Simba”, wikiendi iliyopita liliitikisa miji ya Kilwa, Lindi, Masasi na Liwale katika maonyesho ya sikukuu ya X-Mas.

Disemba 23 Mashauzi walitesa katika ukumbi wa Miwa Pub ndani ya Kilwa kabla ya kuhamia Lindi siku iliyofuata ambapo ilitandikwa show matata katika ukumbi wa Bwalo la Polisi.

Siku ya Xmas Disemba 25 Mashauzi Classic wakaiteka Masasi kwa show iliyopigwa kwenye ukumbi wa Rock City kabla ya kuelekea Liwale katika show ya Boxing Day ndani ya ukumbi wa Tengeneza.

Shuhudia mapicha mapicha kibao ya ziara hiyo ya Mashauzi Classic ndani ya Kilwa, Lindi, Masasi na Liwale.
 Kilwa ila uhondo wa Mashauzi Classic
 Mambo yalivyokolea Kilwa
 Hashim Said ndani ya Kilwa
 J Four Boya akiwapagawisha mashabiki wa Kilwa
 Kali Kitimto na kinanda chake Kilwa
 Mashabiki wa Kilwa
 Abdumalik na mashabiki wake wa Kilwa
 Isha Mashauzi katika onyesho la Kilwa
Aziza Kilwa moja
 Hashim Said akifanya vitu vyake Lindi
 Isha Mashauzi akitumbuiza Lindi
 Asia Mzinga ndani ya Lindi
 Lindi mambo yalikuwa kama hivi
Rahma Aman katika onyesho la Lindi
 Abdumalick akifanya yake Masasi

 Asia Mzinga katika show ya Masasi
 Aziza akijiachia kwa raha zake
 Hashim Said ndani ya Masasi
 Isha Mashauzi akiwapa raha mashabiki wa Masasi
 J Four Boya akikamua bass gitaa
 Kali Kitimoto 'akiwakimbiza' Masasi
 Masasi hiyo
 Isha ndani ya Masasi
 Rahma Amani akikamua mjini Masasi
Waimbaji wa Mashauzi ndani ya Masasi
 Hivi ndiyo Liwale ilivyoitika
 Isha Mashauzi akisepa na kijiji huko Liwale
Vijana wa shoka Mkude Simba (kushoto) na Kali Kitimoto baada ya kumaliza show ya Liwale
-->

No comments