Habari

REAL MADRID HALI TETE LA LIGA …ZIDANE AKALIA KUTI KAVU, ATETA NA WACHEZAJI WAKE

on

Real Madrid imepoteza uwezekano wa kutetea taji la La Liga baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Celta Vigo.
Mabingwa hao watetezi wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamekusanya jumla ya pointi 32 wakiachwa na vinara Barcelona kwa tofauti ya pointi 16.
Kufuatia sare hiyo, kocha Zinedine Zidane amezidi kuingia kwenye tishio la kupoteza kibarua chake na baada ya mchezo huo alilazimika kuwa na kikao kirefu na wachezaji wake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, hatua iliyomfanya achelewe mkutano wa kawaida wa waandishi wa habari.
Daniel Wass aliifungia Celta Vigo bao la kwanza dakika ya 33 lakini Gareth Bale akafunga magoli mawili ya haraka haraka dakika ya 36 na 38 kabla Celta Vigo hawajazawazisha dakika ya 82 kupitia kwa Maximiliano Gomez.
Celta Vigo wangeweza kuibuka na ushindi kama penalti yao ya dakika ya 72 iliyopigwa na Iago Aspas ingetinga wavuni.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *