Habari

SAFARI YA ALEXIS SANCHEZ IMEIVA …ARSENAL YAKUBALI YAISHE

on

Alexis Sanchez hajasafiri na timu yake kwenda kuikabili Bournemouth Jumapili mchana hatua ambayo inathibitisha kuwa mshambuliaji huyo wa Chile yuko njiani kutimka Emirates.
Sanchez ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu, anatarajiwa kuhama mwezi huu huku Manchester City na Manchester United zikigombea saini yake.
Juzi kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alikiri kwa mara ya kwanza kuwa Sanchez hataki kusaini mkataba mpya, kauli ambayo inadhirisha kuwa mshambuliaji huyo ni lazima aondoke aidha kwa kuuzwa dirisha hili la Januari au andoke bure mwishoni mwa msimu.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *