SANDTON SOUND KUVAMIA MBAGALA CHAMAZI JUMATANO HII

SANDTON Sound “Wana Lisanga ya Banganga” ambao hivi sasa wanakuja kivingine wakiwa na makali yasiyoshikika, kesho Jumatano wanatarajia kumimina shoo ya kufa mtu ndani ya Teacher’s Pub, Mbagala Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Rais wa Sandton Sound, Mackey Fanta ameinyetishia Saluti5 muda mfupi uliopita kuwa, hii ni mara ya kwanza kwa bendi yao kuvamia viwanja hivyo na kwa hiyo imetokana na maombi mengi ya mashabiki wa maeneo ya Chamazi na Wilaya nzima ya Temeke kwa ujumla.

“Tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye shoo hiyo ambayo ni mwitiko wa maombi yao na ambayo pia imepangwa kuanza kurindima majira ya saa 1:30 na kuendelea hadi majogoo,” amesema Mackey.


Sandton Sound inayotamba kwa kutumbuiza muziki safi inakusanya wanamuziki wengi wenye uwezo wa hali ya juu ambao miongoni mwao ni waimbaji Francis Sheggy, Christian Sheggy, Tabia Batamwanya na Miss Iringa mwaka 2000, Sylvia Mwakilufi.

No comments