SIKINDE KUFUNGUA MWAKA NA KIBAO KIPYA STUDIO... ni "Naisubiri Bahati", makucha ya Habib Abbas Jeff

WAKATI wowote kuanzia dakika hii, Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae” wataingia Studio ya Sound Crafters kurekodi kibao chao kipya cha “Naisubiri Bahati” ambacho ni makucha ya mcharazaji ngoma mkongwe, Habib Abbas Jeff.

Kiongozi mwandamizi wa Sikinde, Abdallah Hemba ameitonya Saluti5 kuwa, kila kitu kimeshakamilika kuhusiana na matayarisho hayo ya kuingia Studio ambapo kinachosubiriwa sasa ni ratiba na nafasi ya mtayarishaji wa Sound Crafters ambaye ni Enrico.

Hemba amewataja wanamuziki watakaoshiriki kurekodi kibao hicho kuwa ni pamoja na waimbaji Hassan Bitchuka, Musemba Minyugu, Said Msakara, Karama Regessu, Hassan Kunyata pamoja nay eye mwenyewe, (Hemba).


Wengine ni wapiga ala Ramadhani Mapesa (gitaa la Solo), Steven Maufi (Rythm), Mjusi Shemboza (Bass), Habib Jeff (Drums), Omary Jamwaka (Tumba) na Mbaraka Othman, Hamis Milambo pamoja na Shaaban Lendi kwenye ala za upepo. 

No comments