SINZA SOUND BAND YAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA MASHABIKI WAKE


SALAMU za mwaka mpya zimeendelea kumiminika kutoka kwa wasanii na wadau, baada ya bosi wa Sinza Sound Band, Said Kaunga kuwatakia “mwaka mpya mwema” mashabiki wote wa bendi yake na muziki wa dansi kwa ujumla.

Katika salamu hizo, kaunga amesema kuwa anashukuru kuona mwaka 2017 umemalizika salama kwa upande wa bendi yake, huku akiwahakikishia mashabiki kuwa mwaka huu wa 2018 utakuwa wa kiburudani zaidi.

“Nawashukuru mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi kwa kuwa pamoja na sisi kwa kipindi chote cha mwaka 2017, naomba niwaahidi kuwa mwaka huu tutawazidishia vituz na majamboz zaidi ili kuendelea kuwavuta,” amesema Kaunga.


“Nawaomba muendelee kutuunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi kila tutakapokuwa tunafanya shoo, hususan pale Lion Hotel tunakotumbuiza kila wiki katika siku za Ijumaa na Jumamosi,” ameongeza bosi huyo mahiri kwa uimbaji. 

No comments