Habari

TOTTENHAM YAAMUA KUBORESHA MASHARA WA HARRY KANE

on

Tottenham itamfanya Harry Kane kuwa mchezaji raia wa England anayelipwa pesa ndefu zaidi katika Premier League.
Wakati Raheem Sterling wa Manchester City ndiye Mwingereza anayelipwa pesa nyingi kwa sasa akipokea pauni 180,000 kwa wiki, Tottenham inaandaa dili jipya kwa Harry Kane litakalowingizia pauni 200,000 kwa wiki.
Kane anapokea pauni 110,000 kwa wiki katika mkataba wake wa sasa akiwa anashika nafasi ya 35 katika orodha ya wachezaji wanaolipwa pesa nyingi Premier League.
Real Madrid inatajwa kumwinda Harry Kane lakini Tottenham imeamua kuubomoa mfumo wake wa mshahara ili kuhakikisha inaendelea kuwa na kinara huyo wa upachikaji wa magoli.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *