WANINGA AUFAGILIA MUUNGANO WAKE NA SALLEH KUPAZA NDANI YA IVORY BAND

MCHARAZAJI ngoma mahiri, Hamza Salleh “Waninga” amesifu muungano wa bendi yake na ile ya mwimbaji Salleh Kupaza ya Ivory Band akisema ndio muungano wa kweli na uhakika.

Waning amesema kuwa, lengo lao la kuungana ni kuhakikisha wanatengeneza grupu ambalo litakuwa mfano bora kwa makundi mengine yote ya muziki Bongo.


“Kwa sasa tupo Tunduru tumeweka kambi na mimi nimeshatoa zawadi ya 2018 kwa mashabiki wetu, nimetunga wimbo wa miondoko ya singeli ya ukweli na sasa imekua gumzo Tunduru nzima,” amesema mwanamuziki huyo.

No comments