WANINGA, KUPAZA WASEMA: "TUTAKUJA KUHESHIMIANA TU MJINI"

MMOJA wa mabosi wa bendi ya Ivory, Hamza Salleh “Waninga” amesema kuwa bado wanaendelea na kambi ya mazoezi Tunduru mkoani Songea huku akisisitiza kuwa wanachokifanya huko ni kitu kitakachokuja kuleta “heshima” jukwaani.

Waninga aliyekuwa mkurugenzi wa bendi ya W Music, hivi karibuni aliamua kuungana na nguli Salleh Kupaza katika bendi yake ya Ivory ambapo sasa wanaendelea kupika vibao vipya kwa ajili ya albamu yao ya kwanza ya pamoja.


“Nataka kila mtu ajue kwamba tunachokifanya huku sio kitu cha kitoto, sisi ni watu wazima ambao tunauchukulia muziki kuwa ni kazi na sio ubishoo kwahiyo tuko tunafanya mambo ambayo yatakuja kuwakimbiza watu mjini tutakapoanza mambo yetu jukwaani,” amesema Waninga.

No comments