Habari

WENGER ASEMA HANA MPANGO WA KUTIMKA ARSENAL MSIMU UJAO …asema hajawahi kuvunja mkataba katika historia yake

on

Licha ya wengi kuamini kuwa Arsene Wenger atatimka Emirates mwishoni wa msimu huu, kocha huyo amesisitiza kuwa atakuwepo Arsenal msimu ujao.
Hatma ya Wenger ipo mashakani baada ya mwendo wa kusuasua msimu huku ikishinda mechi moja tu katika michezo yake sita ya mwisho.
Mfaransa huyo alisaini mkataba wa miaka miwili mwanzoni mwa msimu huu ambapo ndani ya dili hilo, hakuna dau lililowekwa kwaajili ya yeye kuvunja mkataba huo.
Alipoulizwa siku ya Ijumaa iwapo yuko mbioni kutimka Arsenal, kocha huyo alisema: “Nitakuwa hapa msimu ujao, mkataba wangu unadhihirisha hivyo, sijawahi kuvunja mkataba katika historia yangu na sina nia ya kufanya hivyo”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *