YAH TMK KUSHEREHEKEA BIRTHDAY PART YA BOSI WAO JUMAMOSI HII BULYAGA BAR

KAMA ilivyo kawaida yao kwa kila wiki, Yah TMK Modern Taarab Jumamosi hii wanatarajiwa kuliamsha dude pale Bulyaga Bar Temeke kuanzia milango ya saa 3:00 usiku na kuendelea hadi mida ya mswaki.

Katika shoo ya Jumamosi hii am bayo wanaume watadondosha mtonyo wa buku tano mlangoni na wanawake watapenya kwa hati punguzo ya sh. 2000, Yah TMK watasherehekea kukata keki ya birthday ya meneja wao ambaye pia ni rais wa Usher Family na meneja wa Bulyaga, Muddy K.

Meneja wa Yah TMK, Said Kessy Mnyama amewaomba mashabiki wao wote kujitokeza kwa wingi kwenye shoo hiyo kufaidi mambo matamu waliyowaandalia ikiwa ni pamoja na vibao vyao vipya ambavyo bado havijasikika kokote.

No comments