Habari

YAH TMK WASEMA MWAKA 2018 NI MWAKA WAO KIBURUDANI… wawataka mashabiki kukaa mkao wa kula

on

MMOJA wa viongozi waandamizi wa Yah TMK Modern Taarab, Father
Mauji amewaomba mashabiki wao kukaa mkao wa kusubiri burudani ya uhakika zaidi
katika mwaka huu mpya wa 2018.
Mauji ambaye ni mkali wa kucharaza gitaa kiongozi la Solo,
amewataka mashabiki kutoyatilia maanani maneno yanayotupiwa mitandaoni kuhusu
kuwavurugia akisema kuwa ni uzushi usio na maana.
“Mashabiki wetu wa Yah TMK tegemeeni mambo mazuri zaidi kutoka
kwetu, msiyumbishwe na mambo ya kwenye mtandao sisi tupo kikazi na inshallah hivi
karibuni mtapata nyimbo zetu mpya hii itakua ni zawadi ya mwaka mpya kwenu
mashabiki, please tunawaomba mzidi kutusapoti,” amesema Father Mauji.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *