AUDIO: SIKILIZA NAMNA ALLY STAR ALIPOTHIBITISHA UMASIKINI HAUMPENDEZI MTU MWAKA 1995 KWENYE 'NATANGA NA NJIA'


MWAKA 1995 TOT Taarab iliachia wimbo wa ‘Natanga na Njia’ ambao leo Saluti5 inakupa fursa ya kuburudika nao ili kujikumbushia namna mtunzi Ally Hemed Star alivyoambaa na ghani za kusisimua katika wimbo huu.

Meseji katika wimbo huu ni namna ufukara usivyoweza kumpendeza mtu kama tai, ambapo mwimbaji analalamika kwa anavyoona maisha yanamwendea kombo , hasa kutokana na kukimbiwa hadi na ndugu na marafiki.


Walioshiriki katika ala kwenye wimbo huu ni Hamad Mperembe (Gitaa la Solo), Said Mpiruka (Rhythm) na Khatibu Kitia (Bass), wakati kwenye kinanda amesemama Juma Jerry, Drums Patrick Thomas, Mzee Issa (Tumba) na Merikion Komba amekung’uta ‘Magoma mwitu’.

No comments