BIRTHDAY PARTY YA LUIZER MBUTU HAPATOSHI THE JONZ MAGOMENI MWEMBECHAI

JUMAMOSI hii The Jonz, Magomeni Mwembechai kunatarajiwa kuwaka moto pale African Stars Band ‘Twanga Pepeta’ watakapowasha moto mkali wa burudani katika ‘Birthday Party’ ya mwimbaji wao mwandamizi, Luizer Mbutu.

Mashabiki 100 watakaowahi kuingia ukumbini kwenye shoo hiyo ambayo kiingilio chake ni sh. 7,000 kwa wanaume na 5,000 kwa upande wa kinadada, watazawadiwa zawadi ya CD ya audio ya Twanga Pepeta.


Vibao vyote vikali vya wakongwe hao wanaotikisa jiji na nchi nzima kwa ujumla hivi sasa, vimepangwa kutumbuizwa katika mtindo wa bandika bandua ili kukata nma kunmaliza kabisa kiu ya mashabiki watakaohudhuria.

No comments