INSPECTOR HAROUN, PASHA, HANIFA MAULID WAUNGANA NA NTAMBA BAND VALENTINE DAY

WASANII Inspector Haroun, Pasha na Hanifa Maulid wanaungana na Ntamba Band Jumatano, Februari 14 katika kusherehekea sikukuu ya Valentine ambapo wanatarajiwa kukinukisha ndani ya Mpo Afrika, Tandika Devis Corner, jijini Dar es Salaam.

Mtonyo wa buku tano tu ndio umepangwa kuwa kiingilio katika shoo hiyo ya kijanja ambayo itaanza kumiminwa majira ya saa 2:00 usiku na kuendelea hadi majogoo.


Kampuni ya Nyegera Waitu Entertainment inayoandaa shoo hiyo imeahidi burudani ya uhakika kwa watakaohudhuria ambapo wasanii wote watapanda jukwaani kwa zamu kutumbuiza katika mtindo wa bandika bandua kuanzia mwanzo hadi mwisho.

No comments