JADO FFU AHAHA KUWAUMBUA WANAOMWOMBEA MABAYA NA OG DAR MUSICA YAKE

JADO FFU amesema kwamba anachowaza sasa ni kuzidi kusonga mbele akiwa na bendi yake ya Original Dar Musica ili kuepuka kuwapa maadui nafasi ya kumcheka pindi ikitokea kuporomoka.

Akipiga stori na Saluti5, Jado amesema kuwa vita alivyokuwa akipigwa na baadhi ya wamiliki wa bendi nyingine kabla hajasajili rasmi bendi yake hiyo, vinamtisha na kumfanya awe na tahadhari kubwa akiamini kuna kundi la watu wanaokesha kumwombea atetereke.

“Nikikumbuka siku niliyokamilisha usajili wa bendi yangu na nikikabidhiwa vyeti vya umiliki huwa machozi yananitokaga kwa jinsi nilivyokuwa napigwa vita na baadhi ya wamiliki wa bendi nyingine na hata baadhi ya wanamuziki wenzangu,” amesema Jado.

“Wengine walikuwa wakinidhihaki na kusema sitoweza ila mpaka leo bado nimesimama imara. Sina la kuongea zaidi ya kusema asante Mungu na pia asanteni wadau wote mliokuwa bega kwa bega na mimi kwani bila ya ninyi naamini nisingefika popote,” ameongeza mwanamuziki huyo.

No comments