PICHA 14:BIRTHDAY PARTY YA LUIZER MBUTU FUNIKA MBAYA THE JOHS MWEMBECHAI


JUMAMOSI African Stars Band ‘Twanga Pepeta’ imepiga shoo maalum iliyopewa jina la ‘Birthday ya Luizer Mbutu’, ndani ya The Johs Magomeni Mwembachai, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mashabiki wengi zaidi wa miondoko ya dansi.

Mbali ya burudani kali ya nyimbo mbalimbali zilizosisimua wengi, waliohudhuria walifaidi ‘vibweka’ vya hapa na pale vilivyokuwa vikifanywa na wasanii wa Twanga Pepeta ambavyo kwa namna moja ama nyingine navyo vilikuwa kivutio tosha.


Pata picha 14 za namna mambo yalivyokwenda jukwaani kwenye shoo hiyo.
 Mwimbaji Kalala Junior akirapu huku mnenguaji wa Twanga Pepeta akionyesha ufundi wake wa kunengua 
 Luizer Mbutu akifafanua jambo wakati 'shughuli hiyo ikiendelea
 Hapa wanenguaji wa Twanga Pepeta wakipagawisha mashabioki wao kwa shoo kali
 Rapa Msafiri Diof akirapu kwa hisia kali
 Miraji Shakashia akicharaza gitaa lake la Solo kwa ufundi mkubwa
 Wanenguaji wa Twanga Pepeta wakiwa kazini
 Bosi wa Aset Entertainment inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka akimlisha keki msanii wake, Luizer 
 Hapa baadhi ya waimbaji na wanenguaji wa Twanga Pepeta wakisubiri kumuimbia 'Happy Birthday' mwenzao, Luizer
 Luizer (kushoto), akimlisha keki mmoja wa wanenguaji wake wa kike
 Hapa ikawa zamu ya Haji BSS kudambulia keki
 Waimbaji Kalala Junior (kushoto) na Luizer wakiwa wamekumbatiana kwa furaha kabla ya kulishana keki
 Shughuli inaendelea
 Keki ikisubiriwa kukatwa
Jojo Jumaine na Kalala Junior wakiwajibika kwa mashabiki wao

No comments